Uongozi wa Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa, Paris Saint-Germain umelaani vitendo vya wafuasi waliodaiwa kukusanyika nje ya nyumba ya Mshambuliaji kutoka Brazil Neymar, na kuimba nyimbo za kumshinikiza aondoke klabuni hapo.

Limekuwa juma la misukosuko kwa klabu hiyo ya jijini Paris ambayo imemsimamisha Lionel Messi kwa muda wa majuma mawili kutokana na kufanya safari ya kwenda Saudi Arabia bila ya kupewa ruhusa.

Mashabiki walirekodiwa nje ya makao makuu ya klabu hiyo wakiimba nyimbo za kuitaka bodi hiyo kujiuzulu haraka iwezekanvyo baada ya kumkosea heshima Messi kufuatia adhabu hiyo.

Messi alikwea pipa hadi Saudi Arabiakutokana na ishu za kibiashara akiwa kama balozi wa nchi hiyo, hata hivyo PSG ilichukizwa na kitendo cha staa huyo kutimka kambini.

Kwa mujibu wa ripoti, Messi aliondoka jijini Paris bila kupewa ruhusa na uongozi wa klabu yake ya PSG, na kutokana na hilo miamba ya hiyo ya Ufaransa imempa adhabu na hataungana na wachezaji wenzake kwa wiki mbili.

Hiyo inamaanisha kwamba Messi atakosa mechi mbili za Ligue 1, PSG itakapomenyana na Troyes mwishoni mwa juma hili na mechi dhidi ya Ajaccio ambao utachezwa Mei 13.

PSG iliandika maneno mazito kupitia mitandao yao ya kijamii ikilaani vikali vitendo hivyo ambavyo vinachochea fujo.

“Klabu ya PSG imechukizwa na inalaani vikali vitendo visivyovumilika na vya matusi vya kikundi kidogo cha watu vilivyofanyika Jumatano, bila kujali tofauti za maoni, hakuna kinachohalalisha vitendo kama hivyo, klabu inatoa ushirikiano kwa wachezaji wote, benchi la ufundi na wote waliosababisha fujo hizo,” PSG iliandika katika taarifa hiyo

Rwanda: Mafuriko yaacha majonzi familia zikiomboleza
Wanne wa familia moja wafariki kwa kujichoma moto Morogoro