Mzigo wa mabunda 50 ya sigara ambayo ni packet 500 zenye uzito wa kilo nane zilizotengenezwa kwa kutumia mmea wa bangi zilizokuwa zikisafirishwa kutoka nchi ya Zimbabwe kuja nchini Tanzania umenaswa na Jeshi la Polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Theopista Mallya amethibitisha kukamatwa kwa Sigara hizo zenye dawa za kulevya na kusema tukio lilitokea April 29, 2023 katika Mpaka wa Tunduma wakati wahusika wakijaribu kuvusha mzigo huo.

Amesema, mzigo huo ulikuwa ukisafirishwa kwa kutumia basi la abiria la Kampuni ya Classic la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC, lenye namba za usajili 6321AA25 lililokuwa likitokea nchini Zimbwabwe kwenda jijini Dar es Salaam.

Aidha, Kamanda Theopista ameongeza kuwa mabunda hayo yalikuwa yamefichwa nyuma ya kiti cha dereva wa basi hilo na kwamba utaratibu juu ya suala hilo unaendelea ili kuwabaini wahusika wote na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Kesi vifo vya waumini: Mchungaji Odero aachiliwa kwa dhamana
Majimaji FC yasubiri hukumu TPLB