Meneja wa Klabu Bingwa nchini England Pep Guardiola amesema mshambuliaji wake kutoka Norway Erling Haaland anastahili kulindwa sana na wachezaji wenzake klabuni hapo baada ya kuvunja rekodi ya kufunga mabao katika msimu mmoja wa Ligi Kuu ‘EPL’.

Haaland alifikisha jumla ya 51 katika mashindano yote juzi Jumatano (Mei 03) usiku, wakati umaliziaji wake mzuri ulipoongeza mabao yake kwenye Ligi Kuu hadi 35 na kuvunja rekodi ya mashindano ya Andy Cole na Alan Shearer.

Mchezaji huyo wa aliyetua Man City mwanzoni mwa msimu huu akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani alifunga pamoja na Nathan Ake na Phil Foden katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya West Ham.

Baada ya mchezo huo, Guardiola alisema Haaland anastahili ulinzi.

“Ilikuwa (maalum), nadhani anasta- hili,” alisema bosi huyo wa City.

“Timu zote zilistahili kwa sababu bila timu asingeweza kufanya hivyo, lakini ni mshambuliaji maalum.”

“Tumefurahishwa sana naye kwa sababu ni mchezaji maalumu. Nadhani kila mtu anafurahi kuwa naye pamoja nasi.”

“Kwa kweli rekodi hii itavunjwa mapema au baadaye, labda naye katika siku zijazo au labda nyingine lakini watalazimika kufunga mabao mengi kwa sababu alifunga mengi.”

Geita Gold yaitega Mbeya City Ligi Kuu
Rwanda: Mafuriko yaacha majonzi familia zikiomboleza