Mabingwa wa Soka nchini Hispania wanapaswa kupewa HEKO kwa kufanikiwa kumpata mrithi kiungo Luka Modric ambaye ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu 2022/23.

Real Madrid jana Alhamis (Mei 04) imeripotiwa kufikia makubaliano binafsi na Kiungo kutoka nchini England na Klabu ya Borussia Dortmund, Jude Bellingham.

Madrid ilimfuatilia Bellingham mwenye umri wa miaka 19, tangu msimu ulipoanza hata hivyo ikapata hofu huenda Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City wangewapindua katika kinyang’anyiro cha kuwania saini yake.

Real Madrid ilifahamu kabisa itakuwa na kazi kubwa ya kumshawishi kiungo huyo aliyeitumikia England wakati wa FAinali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, ili ajiunge nao mwishoni mwa msimu huu.

Huko mjini Madrid Siri imefuchuka ikieleza kwamba, hadi sasa Modric hajasaini mkataba mpya lakini kwa upande wa Toni Kroos ameongezwa mkataba wa mwaka mmoja.

Hata hivyo Modric ameanza kuhusishwa na klabu kutoka Saudi Arabia katika dirisha la usajili mwishoni mwa msimu huu, huku tetesi hizo ziliwahi kusikika mwishoni mwa msimu uliopita.

Lakini endapo Madrid itafanikuwa kunasa saini ya Bellingham atakuwa chaguo sahihi la kuziba pengo la kiungo huyo wa kimataifa wa Croatia mwenye kipaji cha kucheza soka.

Taarifa zimeripoti Madrid ilikuwa katika mazungumzo na Borussia Dortmund kuhusu uhamisho wa kiungo huyo kinda ambaye mwezi ujao atatimiza umri wa miaka 20, kwa mujibu wa mkali wa masuala ua usajili Fabrizio Romano, Bellingham ameonyesha nia ya kujiunga na timu hiyo yenye maskani yake Madrid.

Mbali na Bellingham, Madrid ilihusishwa na viungo kadhaa kama Florian Wirtz wa Leverkusen na Ryan Gravernberch wa Bayern Munich.

TMA yafuatilia mifumo hali ya hewa uwepo mvua za El Nino
Hisa Kiwanda cha Saruji Tanga kaa la moto