Ujumbe wa Maofisa wa Forodha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ukiongozwa na Mkurugenzi wa Forodha na Ushuru wa bidhaa, René Kalala Masimango, umetoa pongezi kwa Serikali na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania – TPA, kwa kuweka mikakati madhubuti ya ujenzi na uimarishwaji wa Bandari Kavu ya Kwala iliyopo Mkoani Pwani.

Masimango anayesimamia Majimbo ya Haut Katanga, Lualaba, Tanganyika na Lomami, ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea Bandari hiyo ili kujionea utayari wake katika utoaji wa huduma.

Amesema, “ tunawapongeza kwa kazi nzuri. Majimbo ninayoyasimamia, Jimbo la Haut Katanga linapokea asilimia 80 ya Shehena ya DRC inayopitia Bandari ya Dar es Salaam, hivyo ni muhimu sana kwetu kufika hapa Bandari kavu ya Kwala ili kuona utayari wake, kutambua na kuelewa kazi zinazofanyika hapa.”

Naye Balozi wa Tanzania nchini DRC, Said Juma Mshana amesema lengo la ziara hiyo ya Kibiashara ni kuona utendaji kazi wa Bandari na kuimarisha Biashara Kati ya Tanzania na nchi hiyo ya Kidemokrasia ya Kongo.

Aidha, ujumbe huo pia umetembelea na kukagua eneo la Hekta 10 lililotengwa na Serikali kwa ajili ya kuhudumia Shehena ya mzigo wa DRC unaopita Katika Bandari ya Dar es Salaam.

Liverpool ina kazi ya kufanya England
Mawaziri wajadili AFCON 2027