Kocha Mkuu wa Simba, Mbrazil Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameanza kuumiza kichwa namna ya kuweza kumdhibiti mshambuliaji wa Azam FC Prince Mpumelelo Dube kwa kuhakikisha hapati nafasi yoyote ya kuweza kufunga bao katika mchezo wao wa Nusu Fainali ya Kombe la FA kwa kuwapa jukumu mazito mabeki wake Enock Inonga na Joash Onyango.

Simba SC itacheza dhidi ya Azam FC mchezo wao wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kesho Jumapili (Mei 07) katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Kocha Robertinho amesema kwa katika maoezi ya mwisho leo Jumamosi (Mei 06) amemaliza kazi ya kumzuia Mshambuliaji huyo kupitia safu yake ya ulinzi ambayo itapaswa kuongeza umakini.

Robertinho amefikia hatua hiyo kutokana na rekodi ya Dube kuweza kuifunga Simba SC katika mchezo ambao anakutana nao kila ambapo mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23 amewafunga mara mbili.

“Tumekamilisha maandalizi kuelekea katika mchezo wetu na Azam kwa sababu tuna matarajio makubwa ya kushinda, lakini lazima tuongeze ukubwa wa umakini kuelekea katika mchezo wenyewe kwa sababu tunaenda kucheza na moja kati ya timu nzuri.”

“Lakini lazima tuongeze umakini hasa kwenye safu ya ulinzi kwa sababu tunaelewa kwa namna wapinzani walivyo bora washambuliaji wao, wanajua nini ambacho wanakifanya sasa ukiangalia rekodi za mechi ambazo zimepita dhidi yao, unaona kuna haja ya kuongeza umakini ambao ndiyo kitu kikubwa ikiwa malengo yetu ni kushinda,” amesema Robertinho

Timu hizo zinakutana huku Azam FC ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza bao 1-0 katika hatua ya Nusu Fainali ya michuano hii msimu wa 2020/21, lililofungwa na mchezaji wake wa zamani, Luis Miquissone baada ya mabeki kuzembea.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Majimaji mjini Songea Mkoani Ruvuma, Miquissone alifunga bao hilo dakika ya 89 baada ya mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Bernard Morrison anayeicheza Young Africans kwa sasa kuanzisha kwa haraka mpira wa kutenga ‘Free-Kick’.

Afua zinazomlinda Mtoto kuimarishwa - Serikali
Liverpool ina kazi ya kufanya England