Takriban Watu saba wameuawa na wengine 22 wametekwa nyara katika mashambulizi mawili tofauti huko jimbo la kaskazini mashariki la Borno nchini Nigeria.

Ukosefu wa usalama unaongeza wasi wasi katika taifa hilo lenye watu wengi barani Afrika, wakati Rais mpya akitarajiwa kuapishwa mwezi Mei, 2023 baada ya kushinda uchaguzi ulioibua utata kwa kwa upinzani.

Siku ya Alhamis (Mei 3, 2023), wakulima watatu waliuawa na wengine 11 walitekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa ni wanajihadi wa Islamic State West Africa Province (ISWAP), karibu na kijiji cha Bulayobe.

Wakulima hao, waliingia kilomita 10 nje ya Banki kusafisha mashamba kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa kupanda mazao wakati mvua za msimu zinaxotarajiwa kuanza baada ya siku kadhaa.

Hugo Lloris kuikacha Tottenham Hotspur
Kocha Singida BS aiweka kiporo Young Africans