Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo amezindua kiwanda kidogo cha bidhaa za ngozi na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha kunenepeshea mifugo katika Halmashauri ya Kishapu mkoani Shinyanga.

Akizungumza na wananchi wakati ziara hiyo, Dkt. Jafo ameonesha kuridhishwa na utekelezaji huo wa miradi na kusema imeendana na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali.
 
Amesema, Serikali imedhamiria kuwahudumia wananchi na kuhakikisha wanakuwa na maisha bora kupitia miradi inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

“Ndugu zangu wana Kishapu hongereni sana kwa miradi hii na mmezitendelea haki fedha alizozileta hapa Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na niwaahidi tutaendelea kuwaunga mkono,” amesisitiza Waziri Jafo.

Akiwa katika eneo hilo, pia alikagua lambo la kukusanyia maji, miradi ambayo inatekelezwa kupitia Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Charles III rasmi sasa ni Mfalme wa Uingereza
Rais Samia angoza kikao mchakato Katiba mpya