Bondia Iddi Pialali anatarajia kupambana kuzichapa na Bondia Simon Ngoma kutokea nchini Zambia katika pambano lisilokuwa na Ubingwa.

Meneja wa Pialali, Haider Nurdin amesema kuwa pambano hilo linatarajiwa kufanyika Mei 27 katika ukumbi wa Next Dool Arena uliopo Msasani jijini Dar es salaam.

Amesema Pialali amekuwa akifanya mazoezi kila siku kuwa kwenye hali nzuri ya kushinda pambano hilo.

“Tulipotazama rekodi za mpinzani wetu bondia wangu mwenyewe alikubali kwamba anaenda kupambana na mtu,”amesema Nurdin.

Bondia Ngoma amekuwa akifanya vizuri katika mapambano yake, ambapo ameshinda jumla ya mapambano saba manne kati ya hayo ameshinda kwa K’O, huku akipoteza pambano moja.

Mahakama yataja siku usikilizaji kesi ya Mchungaji Odero
Kocha Julio matumaini kibao Ligi Kuu