Nahodha wa Kikosi cha Marumo Gallants Lehlogonolo Nonyane ameitolea maneno ya shombo Young Africans kuelekea mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Nusu Fainali, Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Marumo Gallants wanaotarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam leo Jumatatu (Mei 08), watakuwa wageni wa Young Africans keshokutwa Jumatano (Mei 10) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, kabla ya timu hizo kukipiga tena Afrika Kusini Mei 17.

Nonyane ametoa kauli ya shombo dhidi ya Young Africans kabla ya kuanza safari ya kuondoka Afrika Kusini kuelekea Dar es salaam tayari kwa mchezo wa Mkondo wa kwanza wa Nusu Fainali.

Nonyane anayecheza nafasi ya ulinzi amesema wanakwenda Tanzania kupambana na Young Africans, lakini wanaamini wapinznai wao sio timu ya kuwatisha, hivyo watapambana na kushinda ugenini kabla ya mchezo wa Mkondo wa Pili ambao utachezwa kwao Juma lijalo.

“Young Africans hawana kitu cha kutufanya tuogope kucheza nao, bado ni timu ndogo kwenye mashindano ya CAF kwa hiyo sisi tunajua tunaenda kushinda.” amesema Lehlogonolo Nonyane

Marumo Gallants wanaelekea Tanzania wakiwa na machungu ya kupoteza mchezo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini 2-0 dhidi ya Mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns mwishoni mwa juma lililopita.

Younga Africans wao wanachagizwa na ushindi wa 2-0 walioupata katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Stars iliyokuwa nyumbani Uwanja wa Liti mjini Singida.

Serikali yaendelea kutoa somo athari matumizi ya Zebaki
Yericko Nyerere: Mo Dewji fukuza wababaishaji Simba SC