Umoja wa wastaafu Tanzania – REAT, umeishauri Serikali kufanya marekebisho ya pensheni za wastaafu wanazozipokea kila mwezi ili waweze kupata fedha ambazo zitawawezesha kujikimu na kupata mahitaji ya msingi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Rais wa umoja huo, Dauda Buikesi akiwa mjini Bukoba amesema kuwa kwa sasa wastaafu wanapokea fedha kiduchu kama pensheni ya kila mwezi na hii inatokana na wastaafu kustaafu utumishi wa umma ikiwa wana mishahara midogo huku wengine wakicheleweshewa malipo yao kutokana na waajiri wao kuchelewesha taarifa za malipo kwa mifuko husika.
Amesema, “changamoto kubwa inayojitokeza ni kwamba wastaafu wanafikia wakati wa kustaafu mwajiri hajapeleka michango yake na mwanachama huyo kwenye mifuko husika, matokeo yake mstahafu huyu anashindwa kupata pensheni yake kwa wakati kwasababu mfuko unasema nakupa fedha kutokea wapi wakati mwajili wako hajazileta.”
Rais wa Umoja wa Wastaafu Tanzania – REAT, Dauda Bilikesi, (kushoto), akizungumza na Waandishi wa Habari.
Dibentious Kamaleki, ambaye ni mwalimu mstaafu pia mwanachama wa umoja wa wastaafu Tanzania – REAT, amesema “kweli nilipata adha kwasababu wakati huo hauna hela yoyote huna kipato, wengine tumestaafu bado tunasomesha kwakweli inakuwa ni matatizo hiyo inaathiri wastaafu.”
Baadhi ya wastaafu waliohudhuria kwenye mkutano huo wameiomba serikali kuingilia kati suala la bima za afya kutokana na wanazozitunia kwa sasa kutokubalika na kutibu baadhi ya magonjwa, wakati kipindi chao utumishi wa umma, hawakuwahi kukutana na changamoto hiyo.