Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amewataka wakandarasi waliopewa kandarasi ya miradi ya maji chini ya wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini – TARURA, kuhakikisha wanasimamia vyema miradi hiyo, ili iwasaidie wananchi na wao kulinda mikataba yao.

Chalamila, ameyasema hayo wakati wa utiaji saini kwa wakandarasi hao ofisini kwake, ambapo pia amewasisitiza kutumia nguvu kazi watu wenye uaminifu watakaoweza kulinda mali za ujenzi wa miradi hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila akiongea na wakandarasi wa miradi ya maji vijijini kwenye ofisi yake zilizopo wilaya ya Bukoba.

Amesema “msiweke vijana wezi, unaweza kuweka kijana site na akakuharibia akaishia kula akaishia kukuharibia kazi, anakaribisha vibaka wanakuja kuiba kwahiyo tafuteni faida kidogo kwa kuweka watu ambao ni safi.”

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Mkoa wa Kagera, Warioba Sanya ameeleza kuwa mkoa wa Kagera umetekeleza kwa wastani wa utoaji maji kwa wananchi ni asilimia 77 na kuwa karibu asilimia 20 itaongezeka mara baada ya miradi hiyo kukamilika.

Meneja wa RUWASA na miongini mwa wakandarasi wa miradi ya maji wakitia saini kwenye ofisi za Mkuu wa mkoa wa Kagera.

“Kwahiyo ukiangalia hapo tutaenda mpaka 89% mpaka 90% ya maji vijijini tukijali miradi yetu vizuri ikaisha kwa ubora hii tunayosaini mwaka huu na ya mwaka jana inayoendelea tukiimaliza tutakuwa tumefikia malengo na irani ya uchaguzi ya chama kinachotuweka sisi kutekeleza kama serikali,” amesema.

Jumla ya miradi iliyosainiwa mikataba na inayoenda kutekelezwa na wakandarasi hao chini ya RUWASA kwenye wilaya zilizopo mkoa wa Kagera itagharimu kiasi cha Shilingi 7.56 Bilioni.

Mwakinyo aporomoka viwango Afrika, Duniani
Ahmed Ally: Tumezomewa kutoka Mtwara hadi Dar