Uongozi wa Klabu ya KMC, umesisitiza malengo yao kwa sasa ni kuitoa timu hiyo kwenye nafasi mbaya waliyopo na kuiweka sehemu salama zaidi ya kuepuka kushuka daraja.

KMC inashika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, ikiwa imeshinda michezo sita, sare nane na kupoteza 18, ikikusanya alama 26, ikishuka dimbani mara 27, bado mechi tatu kumaliza msimu.

Afisa Habari wa KMC, Christina Mwagala, amesema: “Malengo yetu ni kushinda mechi zote zilizobaki ili kutoka nafasi mbaya tuliyopo na kukaa nafasi za juu.

“Tangu tunaanza msimu malengo yetu ni kumaliza katika nafasi za juu ambazo ni nafasi nzuri ambayo haina presha ya kushuka daraja.

“Tunajua michezo iliyobaki ni migumu kwetu, tutapambana kwa hali na mali ili kufanya vizuri japo ligi kwa sasa ni ngumu, kila timu inahitaji kupata matokeo mazuri, hivyo na sisi tutapambana.

Mayele awaita Mashabiki, Wanachama kwa Mkapa
Serikali yaweka wazi kukamilika kwa rasimu sera ya mafunzo