Serikali kupitia Wizara ya Elimu imeweka wazi kukamilika kwa Rasimu ya sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023, inayolenga kuhakikisha elimu inayotolewa inaongeza ujuzi.

Akizungumza na Waandishi wa habari hii leo Jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema, “Rasimu za mitaala ya elimu ya awali, msingi, sekondari na vyuo vya ualimu ambayo inakidhi maelekezo ya Rais wetu nayo imekamilika, Serikali imeamua kutoa rasimu hizi ili kupata maoni ya mwisho ambayo tunataka yawe yashapokelewa ifikapo 31 Mei 2023.”

Ameongeza kuwa, Serikali imeandaa semina ya kuwapitisha wadau katika rasimu hizo ikiwemo kwa wabunge kupitishwa kwenye rasimu hizo za mapitio ya sera na Mitaala mipya itakayofanyika may 10, 2023,  aidha may 12 – 14, 2023.

“Hadi kufikia may 31, 2023, Mwanzoni tulipokea maoni bila kuwa na rasimu tukayachambua na kufanyia kazi, tumeyachakata maoni hayo na tumetengeneza Rasimu ya Umma wa Watanzania ili watolee maoni kwenye ambayo tutayaingiza kwenye michakato ya maamuzi,” amesema Prof. Mkenda

Aidha amesema Wanaotaka kuhudhuria kongamano hilo wanakaribishwa kujisajili ambapo Tangazo la kualika kujisajili linaanza kutoka leo na utaratibu wa kujisajili wa kujisajili utatangazwa lakini Wapo wataalamu na wadau mbalimbali wamepewa mwaliko Rasmi kuja na tutajitahidi kulitangaza kongamano hili ili kila mtu asikilize maoni yanavyotolewa.

 “Watanzania wote popote walipo wanakaribishwa kupitia rasimu hizi na kutoa maoni zao, Rasimu hizi zinapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo, na Tovuti ya Taasisi ya Elimu Tanzania”, amesema Prof. Mwaikenda

Naye, katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Mialiko hiyo ipo ndani na nje ya Tanzania ambapo Watanzania wanaoishi nje ya nchi wamealikwa na kutakua na utaratibu maalumu wa kushiriki mjadala huo na kutolea maoni.

Alama tatu zinavyoishurutisha KMC Ligi Kuu
Waitara aishitaki Serikali Tarime, asusia kikao