Waziri Mkuu wa zamani wa Burundi, Alain Guillaume Bunyoni amefikishwa mahakamani akituhumiwa kuhatarisha usalama wa taifa na kumkashifu rais baada ya kukamatwa mwezi uilipopita (Aprili).

Bunyoni alikuwa waziri mkuu kuanzia katikati ya mwaka 2020 hadi Septemba 2022, lakini alifutwa kazi baada ya Rais, Evariste Ndayishimiye kuchukua madaraka.

Aidha, Bunyoni pia aliwahi kuwa Mkuu wa zamani wa Polisi na Waziri wa zamani wa Usalama wa ndani, nafasi yake ya Waziri Mkuu ilichukuliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa wakati huo Gervais Ndirakobuca, siku chache baada ya Ndayishimiye kuonya juu ya njama ya kumuondoa madarakani.

Alisikilizwa na jopo la majaji wa kitengo cha mahakama ya juu ambao waliamua awekwe kizuizini katika jela ya mkoa wa Ngozi uliopo kaskazini mwa Burundi, kabla ya kesi yake kuanza akituhumiwa pia kuhujumu uchumi wa taifa na kupata utajiri kwa njia haramu.

Sakata la kumkashifu Waziri, mpinzani apewa kifungo
TAMISEMI yakanusha taarifa za kujiuzuru kwa Dkt. Dugange