Mahakama nchini Senegal imemhukumu Kiongozi wa upinzani, Ousmane Sonko kifungo cha nyumbani cha miezi sita katika kesi ya rufaa ya kashfa inayomkabili, hukumu ambayo inaweza kukwamisha mpango wake wa kuwania urais mwaka ujao.

Sonko, mwenye umri wa miaka 48, alipata nafasi ya tatu katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2019 na ana nia ya kugombea tena mwaka 2024, lakini kesi mbili zinazomkabili Mahakamani zinaweza kumzuia asigombee.

Alihukumiwa kifungo cha nyumbani cha miezi miwili na kulipa faini mwezi Machi kwa kumkashifu Waziri wa Utalii, Mame Mbaye Niang, na Mahakama ya rufaa ya mjini Dakar iliongeza kifungo hicho hadi miezi sita, hukumu ambayo inaweza kupelekea asigombee urais.

Msemaji wa chama cha Sonko, Ousseynou Ly na wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii walisema hukumu hiyo inaweza kukwamisha mpango wake wa kuwania uongozi kama itatekelezwa, huku mawakili wa mwanasiasa huyo wakiondoka Mahakamani bila kusema lolote.

Polisi wa Tanzania kupata mafunzo nchini Korea
Waziri Mkuu mstaafu afikishwa Mahakamani kwa utajiri haramu