Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema kitendo cha Mbunge wa Tarime Vijijini (CCM) Mwita Waitara kuvua koti na tai akiwa ndani ya Bunge, ni utovu wa nidhamu na kwamba kitendo hicho hakiruhusiwi.

Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo usiku wa Jumanne, Mei 9, 2023 ambapo mbali na kuvua koti na tai Bungeni, pia Waitara alilia akidai kupewa majibu ya uongo kuhusu fidia ya wakazi wa Tarime, Mkoa wa Mara, waliokuwa wakitakiwa kupisha mgodi wa Barrick North Mara.

Amesema, Waitara kama hakuridhika na majibu ya majibu kanuni ziko wazi lakini hakufanya hivyo na kuamua kutoka ukumbini akiwa amevua koti na tai kinyume na kanuni zinavyoelekeza jinsi ya kuvaa ndani ya bunge.

“Huko nyuma imewahi kujitokeza mtu anapiga magoti, anapiga sarakasi, sasa hii ya kutoa nguo, hapa hairuhusiwi na isijirudie tena, kama una hasira kazitolee nje,” alisema Dkt. Tulia.

Kompany ajifunga miaka mitano Turf Moor
Ahmed Ally: Sijui watakaosajiliwa Simba SC