Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ameripotiwa kuuomba uongozi wa klabu hiyo kusajili viungo watatu wapya na tayari wamehusishwa na uchaguzi mwingi katika miezi michache iliyopita.

Alexis Mac Allister, Mason Mount na Ryan Gravenberch wametajwa, lakini pia inaonekana Zielinski yupo kwenye rada zao.

Kulingana na ripoti, Liverpool wanafikiria kwa makini kumsajili Zielinski msimu huu na wanapanga kuanzisha mazungumzo kuhusu uwezekano wa kusaini mkataba katika wiki zijazo.

Ripoti hiyo inadai zaidi kwamba Zielinski anakaribia kuingia mwaka wa mwisho wa kandarasi yake ya sasa na hakuna uwezekano kwamba atasaini mkataba mpya.

Kwa hivyo, uhamisho wa majira ya joto unaweza kuwa kwenye kadi na kwa hali hiyo, Liverpool watapewa nafasi nzuri ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland kwa mkataba wa bei nafuu.

Hata hivyo, Meczyki linadai kuwa kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 hatakewa rahisi kwa kikosi cha Klopp kwani Newcastle United pia imekuwa ikionyesha nia ya kumsajili nyota huyo wa SSC Napoli.

Zielinski mwenye thamani ya takriban Pauni 35 milioni amejidhihirishia kuwa mmoja wa viungo bora zaidi wa Serie A tangu ajiunge na Napoli 2015.

Nyota huyo amekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Napoli msimu huu, akiisaidia kushinda Scudetto baada ya miongo mitatu.

Pauni Milion 70 kumng'oa Raphinha FC Barcelona
Man Utd yaitega SSC Napoli kwa Kim Min-Jae