Kutokana na kupata uhakika wa kuendelea kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, viongozi wa Ihefu wameanza kufumua kikosi kwa kushusha mastaa wapya ambao wataongeza ushindani.

Taarifa kutoka Highland Estate zinaeleza kuwa, Viongozi wa Klabu hiyo wapo kwenye mchakato wa kumalizana na washambuliaji Obrey Chirwa, beki David Mwantika na kiungo Papy Tshishimbi.

“Tumepanda msimu huu na tulifikia hatua ambayo haikuwa nzuri kwetu uongozi umewekeza fedha nyingi dirisha dogo kwa kusajili wachezaji wengi ambao hadi tulipo sasa tunawapongeza.”

“Tunapambana kuhakikisha timu inabaki pamoja na kubakiza mechi tatu tuna amini tunaweza kufanikisha hilo hivyo tumeanza kupunguza baadhi ya wachezaji ili tuweze kuongeza wengine ambao wataifanya timu iwe na ushindani,” kimeeleza chanzo hicho

Chanzo hicho kimeendelea kubainisha kuwa, kuna wachezaji wengi wataondoka kwa mujibu wa benchi la ufundi lakini hadi sasa ni majina matatu ambayo tayari yamepitishwa kumalizana nao.

Katibu Mkuu wa Ihefu, Zagalo Chalamila alipotafutwa alithibitisha suala hilo amesema hao bado ni wachezaji wao halali na kuwaacha au kuendelea nao msimu ujao wanaliachia benchi la ufundi.

“Msimu bado haujaisha hatuwezi kuondoa wachezaji katikati ya msimu bado tunawahitaji ili kuipambania timu iweze kucheza ligi msimu ujao, kwa sasa tunasubiri ripoti ya kocha.”

“Kocha bado hajatoa ripoti ya kuwaacha na kusajili wachezaji wengine tayari kwa ajili ya msimu ujao hivyo hatuwezi kuzungumzia suala la usajili sasa hadi msimu utakapomalizika,” amesema.

Chirwa na Tshishimbi mikataba yao inamalizika mwisho wa msimu huu 2022/23, kwani walisaini mkataba wa mwaka mmoja kila mmoja huku Mwantika akiingia dirisha dogo.

Polisi aliyewauwa wageni wawili, kujeruhi auawa
GGML Kili Challenge-2023 kukusanya bilioni 2