Kocha Mkuu wa Simba SC Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameuagiza uongozi wa Simba kusajili wachezaji watano wenye ubora wa hali ya juu ili timu hiyo iweze kugombania mataji katika michuano yote watakayoshiriki msimu ujao.

Simba SC ambayo imeelekea kumaliza msimu wa pili bila kubeba taji lolote ndani na nje ya Tanzania, inahitaji kufanya usajili huo ili kuboresha kikosi chake ambacho kwa mujibu wa kocha huyo raia wa Brazil kimeshindwa kupambana kutokana na kukosa wachezaji bora.

Robertinho amezitaja nafasi ambazo anahitaji kuziboresha kuwa ni mshambuliaji, kiungo mkabaji, beki wa kati, winga na beki wa pembeni mmoja ili waweze kuwa washindani wakweli hasa kwenye mashindano ya kimataifa.

“Kilichotukwamisha msimu huu ni mapungufu yaliyopo ndani ya kikosi chetu, tulikosa wachezaji wenye sifa ya upambanaji hasa kwenye michuano ya kimataifa, hili nitaliweka hata kwenye ripoti yangu baada ya msimu kumalizika,” amesema Robertinho.

Kocha huyo ameeleza kuwa mpira wa siku hizi unachezwa kimbinu zaidi na hiyo inategemea na aina ya wachezaji waliopo kwenye kikosi sasa kukosekana kwa wachezaji wenye viwango kama anaowahitaji ndio kulichangia safari yao iishie njiani.

Robertinho amesema katika hilo hawezi kumtupia lawama mchezaji yeyote sababu waliopo walipambana kadri ya uwezo wao mpaka hapo walipofika na kwake wanastahili pongezi kutokana na kucheza kwa kujitoa katika mashindano yote msimu huu.

Tanzania kupata Trilioni 42.4 za miradi ya mazingira
CAF Super League yaishurutisha Simba SC kusajili