Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC, unaendelea mjadala kuhusu muswada wa udhibiti ulipaji wa mahari kabla ya mwanamke kuolewa badala ya kutoa Ng’ombe na fedha.

Muswada huo, umewasilishwa Bungeni na Mbunge, Daniel Mbau ambaye anataka kiwango cha Mahari cha kuwezesha kuoa kiwe Dola 500, ili kuwawazesha wanaume wengi kuingia katika ndoa.

Hata hivyo, katika aaadhi ya nchi za Afrika, wanaume hutoa ngombe kama sehemu ya utaratibu wa ulipaji wa mahari pamoja na pesa tasilimu kitu ambacho kinadaiwa ama kuwa ni tahamani kubwa au kuwa chini ya kiwango kulingana na nyakati na bei ya mfugo.

Hata hivyo, baadhi ya raia wa DRC wamekuwa na maoni tofauti, wakisema wabunge wanapaswa kushughulikia mambo ya msingi badala ya kujadili mahari ya kuolea kwani jambo hilo linazungumzika kati ya wawili wapendanao na familia zao.

Marcelo Bielsa kuinoa La Celeste
Mashabiki, Wanachama Simba SC waombwa radhi