Wafanyabiashara wa Kariakoo leo Mei 15, 2023 wamegoma kufungua maduka yao huku wakishinikiza Serikali kuingilia kati utitiri wa kodi wanotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amefika katika soko hilo la kimataifa kumaliza mgomo huo wa wafanyabiashara na kuwataka warejee katika biashara zao.

Hiyo ni kutokana na kile walichoeleza kuwa wako tayari kufunga maduka hadi jioni kama hawatasikilizwa huku wakimtaka Rais kuwasikiliza.

Msimamo huo walianza kuuonyesha tangu Makalla akizungumza kwani katika baadhi ya vitu alivyosema wafanyabiashara walikuwa wakitoa sauti za kugomea kile anachokizungumza hasa aliposema kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atafanya kikao na kamati ya wafanyabiashara wa soko hilo siku ya Alhamisi Dodoma.

Hata hivyo wafanyabiashara hao wamesema hawaoni sababu ya wao kumfuata Waziri Mkuu Dodoma badala ya wao kufuatwa Kariakoo.

Mmoja wa wafanyabiadhara ambaye hakutaja jina lake alipopewa nafasi ya kuzungumza ikiwa wanataka kurejea katika biashara alisema lengo lao lilikuwa kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan na si Mkuu wa Mkoa.

“Hawa wote waliokuja tumeshawasikiliza, Waziri wa Fedha ameshatusikiliza na hakuna kilichofanyika,” alisema

Honest Kalisti Mjunbe wa Jumuiya ya wafanyabiashara amesema hakuna kurudi nyuma katika hili waliloanzisha

“Mambo ya siasa kwenye biashara zetu hatuhitaji siasa hazina nafasi, Waziri mkuu si kama hajui, Mwigulu Nchemba si Kama hajui, Mkuu wa Mkoa na Wilaya wanajua lakini hakuna kilichofanyika,”amesema.

“Cha msingi waende wakae kwenye kamati yao sisi maduka tunafunga ili tuonane na Rais Samia Suluhu Hassan,”ameongeza.

Promota: Maandalizi yanakwenda vizuri sana
Usaidizi wa kujiuwa: Bunge lapitisha matumizi ya euthanasia