Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesena endapo kikosi chake kingekuwa katika ubora, basi kulikuwa na kila sababu kwa mchezaji wake Darwin Nunez kufunga mabao 20 msimu msimu huu 2022/23.

Hata hivyo, Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kwa ada ya Pauni 85 milioni alisuasua msimu huu na hadi sasa amepachika mabao 11.

Nunez aling’ara na kufunga mabao dhidi ya timu kubwa kama Manchester City, Arsenal, Newcastle, Napoli, Manchester United and Real Madrid na Klopp anaamini atakuwa hatari zaidi msimu ujao na kumwomba aongeze bidii kwani muda wake utafika tu.

“Anahitaji muda wa kuzoea, kwa kiwango chake msimu huu, angeweza kufunga mabao 15, lakini timu haikuwa katika ubora, hebu fikiria kama Liverpool ingekuwa moto, nadhani angefika mabao 20, Lakini ndio hivyo imetokea, walikuwa na nafasi nyingi za kufunga, tumezungumza kuhusu hili, Nunez bado anahitaji muda,” amesema Klopp.

Liverpool na Manchester City ziliwatala Ligi Kuu England kwa misimu kadhaa, lakini msimu huu Majogoo wa jiji haikuwa kwenye ubora wake kama ilivyozeoeleka.

Ikumbukwe msimu uliopita Man City iliipiku Liverpool kwa tofauti ya alama moja na kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England.

“Kupata alama 90, sio jambo dogo, lakini tutapambana kubaki ‘Top Four’, mambo yalikuwa magumu zaidi na ligi ilikuwa ushindani sana msimu huu,” ameongeza Klopp

Liverpool itacheza baadae leo Jumatatu dhidi ya Leicester City inayopambana kuepuka kushuka daraja msimu huu, lakimi kwa upande wa Klopp anataka ushindi ili iendelee kuipa presha Manchester United kwenye kinyang’anyiro cha nafasi ya nne.

Mipango ya Nabi yabainika Afrika Kusini
Mke wa Thiago Silva akata mzizi wa fitna