Imeelezwa kuwa Mlida Lango chaguo kwa Kwanza Simba SC, Aishi Manula muda wowote mabosi wa timu hiyo watamsafirisha kwenda nchini India kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Mlinda Lango huyo huyo anatarajiwa kurejea uwanjani msimu ujao 2023/24, kutokana na majeraha ya bega yaliyomsababishia aikose baadhi ya michezo ya Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu 2022/23.

Akiwa anauguza majeraha hayo, nafasi yake inashikwa na Mlinda Lango chaguo la Tatu  wa timu hiyo, Ally Salim ambaye alionyesha kiwango bora katika Kariakoo Dabi dhidi ya Young Africans mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika waliocheza dhidi ya Wyadd Casablanca ya Morocco.

Kwa mujibu wa mmoja wa mabosi kutoka Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, amesema muda wowote kuanzia leo Jumatatu, Manula atasafiri kuelekea India kwa ajili ya matibabu.

Bosi huyo amesema kuwa, Manula akiwa huko India huenda akatumia wiki moja kwa ajili ya matibabu kabla ya kurejea nchini tayari kwa ajili ya kujiandaa na Pre Season.

Ameongeza kuwa hivi sasa wapo taratibu za mwisho za kukamilisha safari ya nchini huko tayari kwa ajili ya matibabu, licha ya uongozi upo katika mipango ya kumleta Mlinda Lango mwingine atakayekuja kumpa changamoto.

“Manula muda wowote atasafiri kuelekea nchini India ambako atakaa kwa wiki moja kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya bega aliyoyapata akiwa majukumu ya timu.

“Lengo la kumpeleka huko India ili apone haraka kabla ya kuanza msimu mpya wa msimu ujao ambao tumepanga kuanza mapema.

“Tunafahamu umuhimu wa Manula, hiyo ndio sababu ya kupatiwa matibabu na uongozi, kwani aliumia katika timu, hivyo ni lazima timu imtibie,” amesema bosi huyo.

Akizungumzia hilo Meneja wa Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Ahmed Ally amesema: “Ni kweli Manula yupo katika matibabu, lakini hilo la kupelekwa India lipo kwa uongozi wa juu, taarifa lazima itatolewa.”

Azizi Ki: Msimu ujao nitakiwasha zaidi
Try Again afunguka usajili wa CAF Super League