Uongozi wa Simba SC umeweka wazi kuwa utaingia sokoni kumsaka kiungo mkabaji mwenye sifa kama za Luis Miquissone ambaye alitimkia Al Ahly msimu wa 2021/22 akitokea Msimbazi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdalah, ‘Try Again’ amesema wanahitaji kuwa na wachezaji wenye sifa kama za Luis kwenye eneo la kiungo kwa kuwa waliowaleta bado hawajafanya vizuri.

“Tunahitaji kuwa na wachezaji wazuri kwa kuwa tulishindwa kufanya vizuri baada ya wachezaji waliokuwa kwenye kikosi kama Luis Miquissone na Clatous Chama kuondoka hapo kulikuwa na kazi kwa wale ambao tuliwaleta kuendelea kwenye ule ubora.

“Kikubwa ambacho tunakifanya ni kuboresha kikosi kwa umakini hasa kwa ajili ya msimu ujao na tunajua kwamba kuna makosa yametokea na baadhi ya wachezaji ambao tuliwasajili walishindwa kutupa kile tulichokuwa tunakitarajia mambo mazuri yanakuja,”

Wakati luis Miquissone anasepa Simba SC, alikuwa kwenye ubora wake akiwa na rekodi ya kuwafunga bao bora Al Ahly Uwanja wa Mkapa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika jambo lililowavutia mabosi wa Al Ahly kumsajili.

Bao hilo alilifunga Februari 23 2021 mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa katika hatua ya makundi Simba SC walipokuwa kundi A na vigogo hao wa Afrika.

Baada ya kusepa Simba SC ilikosa taji la ligi, Ngao ya Jamii, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ yote yalielekea kwa watani zao wa jadi Young Africans ambao na msimu huu wametwaa taji la Ligi na Ngao ya Jamii.

Vifo watu 201: Ruto akiri udhaifu wa vyombo vya usalama
Joto la mgomo Soko la Kariakoo lazidi kufukuta