Kiungo wa Manchester United, Marcel Sabitzer, atazikosa mechi zote zilizobaki za Ligi Kuu ya England na fainali ya Kombe la FA itakayochezwa mwezi ujao, kutokana na majeraha ya goti yanayomkabili.

Raia huyo wa Australia mwenye umri wa miaka 29, alijiunga Manchester United kwa mkopo tangu Januari mwaka huu akitokea Bayern Munich.

Mchezaji huyo pia aliukosa mchezo uliopita dhidi ya Wolves ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Taarifa iliyotolewa katika mtandao wa klabu ya Manchester United, imeeleza kuwa kiungo huyo atarudi dimbani msimu ujao baada ya kupona jeraha la goti.

“Ni jambo la huzuni kukosa huduma ya Marcel katika kipindi hiki cha hatua za mwisho za kumalizia Ligi Kuu ya England na Kombe la FA, mchango wake bado ulikuwa unahitajika lakini tunamshukuru pale alipochangia tangu alipojiunga nasi,” ilisema taarifa hiyo.

Machester United imebakiza mechi tatu kabla ya kumaliza msimu huu na inapambana kumaliza katika nafasi nne za juu, pia itacheza fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester City itakayopigwa Juni 3, mwaka huu.

Sheva amtaja Shakho, Mayele Ligi Kuu
Taasisi zitunze kumbukumbu historia ya Tanzania - Dkt. Tax