Klabu ya Manchester City inasherehekea kurejea fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwafunga mabingwa watetezi Real Madrid kwa kufanya vyema katika historia ya klabu hiyo.

Kikosi cha Pep Guardiola kinachofukuzia mataji matatu kiliwafunga mabao 4-0 mabingwa hao mara 14 wa Ulaya katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Etihad juzi, na kukata tiketi ya kutinga fainali itakayochezwa jijini Istanbul, Uturuki kwa ushindi wa jumla ya magoli 5-1.

Ushindi ulikuwa wa wa kuridhisha huku Madrid ikimshukuru golikipa, Thibaut Courtois, kwa kuzuia hatari zaidi kwao.

Bernardo Silva aliiweka City kwenye njia ya kutinga fainali dhidi ya Inter Milan kwa mabao mawili ya kipindi cha kwanza kabla ya Eder Militao kujifunga na Julian Alvarez kuongeza la nne mwishoni mwa mchezo.

City sasa watatumaini kunyanyua kombe hilo na kufanya marekebisho kwa kupoteza kwao katika fainali ya 2021 kama sehemu ya kile ambacho kinaweza kuwa mataji matatu.

Taji la kwanza kati ya hayo linaweza kuja Jumapili ikiwa wataifunga Chelsea na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England na fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester United itakayofanyika Juni 3, mwaka huu.

Guardiola amesema: “Kwenye Ligi Kuu tumekaribia, tunajua tunahitaji mchezo mmoja zaidi. “Tunacheza dhidi ya majirani zetu na dhidi ya timu ya Italia katika fainali. Msimu ni mzuri sana. Tuko karibu na bila shaka tutajaribu.”

Mechi ya nusu fainali ya kwanza ya wiki iliyopita dhidi ya Madrid iliyochezwa kwenye Uwanja wa Bernabeu ilikuwa na ushindani mkali, City walitawala umiliki wa mpira kwa muda mrefu lakini Real walikuwa makini zaidi katika mashambulizi ya kaunta.

Wakati huu City ilikataa kuwaruhusu wapinzani wao kukaa nyuma na kujisikia raha na ku pata presha.

Ushindi huo mkubwa ulifanya kulipiza kisasi kwa City baada ya kupoteza dhidi ya Madrid katika hatua kama hiyo msimu uliopita.

Guardiola alisema: “Ilikuwa ngumu sana kupoteza jinsi tulivyopoteza. Wakati huo tulilazimika kumeza sumu lakini mpira wa miguu na michezo huwa inakupa nafasi nyingine.

“Wakati droo ilipokuwa Madrid, nilisema, ‘ndio naitaka’.

“Kila kitu kilikuwepo, nguvu tuliyokuwa nayo kutoka kwa mwaka wa kukosolewa kama wachezaji kwa kutokuwa na tabia tulipopoteza.”

Jean Balake: Msimu ujao nitakiwasha kweli kweli
Kikwete aipongeza GGML kampeni kudhibiti Ukimwi