Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umesema umepokea taarifa kutoka kwa msimamizi wa jengo la Millennium Towers 2 juu ya kuwepo kwa hitilafu ya kushuka ghafla kwa kipandishi (lift), katika jengo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, James Mlowe imeeleza kuwa inatoa pole kwa wote walioathirika na hitilafu ya kipandishi hicho, iliyotokea katika jengo hilo lililopo Makumbusho jijini Dar es Salaam Mei 24, 2023.

Taarifa hiyo imezidi kueleza kuwa, “PSSSF kama mmiliki wa jengo kwa kushirikiana na msimamizi wa jengo Ms. Prolaty Ltd tunafatilia, kusimamia na kurekebisha hitilafu zozote zilizojitokeza ili wapangaji na watumiaji wa jengo waendelee na majukumu yao kama kawaida haraka iwezekanavyo.”

Hata hivyo, taarifa hiyo imefafanua kwamba Wataalam shirika hilo kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama na msimamzi wa jengo wanaendelea na uchunguzi wa hitilafu hiyo na taarifa za kina zitatolewa huku taarifa za awali zikisema kuna majeruhi saba.

AFCON 2027 yapata baraka za Ikulu
Gatoch: Simba SC nimewasikia, njooni tuongee