Polisi wa kupambana na ugaidi – ATPU, nchini Kenya wameingia katika kanisa la Mhubiri Ezekiel Odero la Kanisa la New Life Center na kuchukua vifaa vyake vya mawasiliano, hifadhi za data za kompyuta, maji ya uzima na vitambaa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mawakili wa Mhubiri huyo, Cliff Ombeta na Danstan Omari, Polisi hao walidai kuchukua na kuvizuia vifaa hivyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi, ikiwa ni siku chache baada ya msajili wa mashirika kutaka kufuta usajili wa kanisa hilo kwa madai ya kutolipa kodi.

Ombeta amesema, “Polisi hawa walikuja kwa kanisa siku ya Jumanne na kuchukua vifaa hivyo wakidai kuwa walikuwa wakivipeleka kwa uchunguzi zaidi na masaibu juu ya Odero sasa yamekuwa mengi majuzi walisema halipi kodi hivyo wanataka kufunga Kanisa.”

Mhubiri huyo, amekuwa akichunguzwa kwa madai ya kuhusishwa na mhubiri tata Paul Mackenzie na mauaji ya Shakahola ya Paul Mackenzie wa kanisa la Good News International na mawakili hao wamesema wataenda Mahakamani kumshtaki Msajili wa mashirika pamoja na afisi yake kwa njama ya kuficha mafaili ya kanisa hilo.

Robertinho kukutana na Skauti wa Simba SC
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 30, 2023