Baada ya aliyekuwa Mtendaji Mkuu FC Bayern Munich, Oliver Khan na Mkurugenzi wa Ufundi, Hasan Salihamidzic kufutwa kazi, Rais wa Bayern Munich, Hainer amethibitisha kuwa Kocha Thomas Tuchel ataendelea kusalia kikosini hapo.

Mabosi hao wawili wa Bayern walifutwa kazi kabla ya mechi ya mwisho ya Bundesliga dhidi ya Koln wakati timu hiyo ikitwaa ubingwa wake wa 11, wikiendi iliyopita.

Taarifa zinaeleza Kuondolewa chanzo cha klabuni hapo ni moja ya mabadiliko ambayo klabu inafanya kuelekea msimu ujao japo inaelezwa ishu ya kuondolewa kwa Kocha Julian Nagelsmann ndiyo imewamaliza kwa upande mwingine.

Rais wa klabu hiyo amesema ataendelea kufanya kazi na Tuchel kwani haoni sababu ya kuondoka hapo.

“Sioni sababu ya sisi tushindwe kuendelea na kocha ambaye tuko naye kwa sasa.

“Tunaamini Thomas Tuchel ni moja kati ya makocha bora ndani ya Ulaya na tayari nimezungumza naye kuhusu hilo na yeye kama kocha amenielewa,” alisema Rais

Tanzania kuwa na umeme kila Kijiji Juni 2024 - Serikali
Erik ten Hag aung'ata sikio uongozi Man Utd