Serikali nchini, imepokea msaada wa paundi milioni tano ambazo ni sawa na Shilingi 15 Bilioni kutoka Serikali ya Ungereza, kwa ajili ya awamu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini – TASAF.
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Dkt. Mwamba amesema utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini Tanzania unaendelea vyema na washirika wa maendeleo wamekuwa wakiendelea kutoa misaada kwa ajili ya mpango huo.
Amesema, pia amekutana na Balozi huyo ili kuangazia wakiangazia masuala ya kunusuru kaya maskini na kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo kati ya nchi hizi mbili uliodumu kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Balozi David Concar, alisema Uingereza ni rafiki mkubwa wa Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo, hivyo nchi yake itaendelea kufanya jitihada za kuhakikisha inatoa mchango wake ili kukabiliana na umasikini na kuboresha hali ya wananchi.
Makabidhiano ya Hati za makubaliano ya msaada huo, yamefanyika jijini Dodoma kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba na Balozi wa Uingereza nchini hapa, David Concar.