Uongozi wa KMC FC umeweka wazi kuwa unatarajia kuwakosa nyota wake wanne ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi hicho kwenye mechi za kumaliza msimu kutokana na kukabiliwa na majeraha.
Afisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amewataja nyota hao kuwa ni Matheo Antony, Ibrahim Ame, Frank Mkumbo na Hance Masudi ambao watazikosa mechi zao mbili zilizobakia kwa ajili ya kumaliza msimu huu.
Mwagala ameongeza kuwa pia klabu hiyo imeondoka jijini Dar kwenda Rukwa kwa ajili ya mchezo wao na Prisons ambao utapigwa Juni 6, katika Uwanja wa Nelson Mandela, mkoani humo.
“Tumeondoka na wachezaji 24 ambao tumefanya nao maandalizi kwa wiki moja tangu ligi iliposogezwa mbele, kila kitu kinakwenda vizuri, hali ya wachezaji ni nzuri, wana morali, kila mmoja yupo tayari kwenda kupambana.”