Mashabiki saba wameadhibiwa kutokana na ubaguzi dhidi ya mchezaji wa Real Madrid, Vinicius Junior.

Vinicius aliwataja wale waliohusika na kejeli za ubaguzi wa rangi huko mjini Valencia wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’.

Wanaume wanne walitozwa faini ya pauni 51,700 (Sh mil 151.2) na kupigwa marufuku ya miaka miwili ya kuingia uwanjani kwa kosa la kutundika sanamu ya Vinicius karibu na uwanja wa mazoezi wa Real mwezi Januari.

Watu hao wanne walikamatwa siku 11 zilizopita na kuachiliwa kwa dhamana na mahakama ya Madrid.

Watu wengine watatu walipigwa faini ya pauni 4,300 (Sh mil 12.5) na kufungiwa mwaka mmoja kwa kutoa ishara za kibaguzi wakati wa mechi ya Real huko Valencia mnamo Mei 21. Watu hao watatu wana umri wa kati ya miaka 18 na 21, polisi walisema.

Vikwazo hivyo vilitolewa na Tume ya Taifa ya Hispania dhidi ya ukatili, ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na kutovumiliana katika michezo.

Vinicius, ambaye alipata kadi nyekundu kwenye mchezo huo ilifutwa na baadae La Liga wakasema ilikuwa kadi iliyotolewa kwa makosa na mwamuzi wa mchezo huo.

Ma' RC simamieni Elimu ya haki, ulinzi wa Wazee - Gwajima
Dar24 yafanikisha zoezi ujenzi visima vya maji Ranchi