Klabu ya Newcastle United inataka kumsajili Beki Harry Maguire kutoka Manchester United kwa mkopo, huku wakijipanga kumnunua jumla, mkopo utakapomalizika.

Beki huyo wa kimataifa wa England ataondoka Old Trafford kama dili litakuwa freshi, ingawa Man United hawana mpango wa kumtoa kwa mkopo Newcastle.

Endapo Newcastle watawasilisha ofa nzuri, Man United wanaweza kumuuza jumla kwani hayupo katika kipango ya Erik ten Hag msimu ujao 2023/24.

Wakati huo huo, Aston Villa wanafuatalia kwa makini mustakabali mzima wa hatima ya Maguire na wana nafasi nzuri ya kumsajili kwa mkopo dirisha hili la kiangazi la usajili.

Tottenham nayo ilihusishwa katika kinyanga’nyiro cha kuwania saini ya beki huyo aliyekosa namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza chini ya Ten Hag.

Maguire alisugua benchi msimu uliopita tangu ujio wa Lisandro Martinez akitokea Ajax na mara nyingi Ten Hag amekuwa akimtumia pamoja na Raphael Varane.

Awali taarifa ziliripoti Maguire angebaki kukipiga Man United msimu ujao, lakini huenda akauzwa.

Sancho yupo hatarini Manchester United
Wandiba apigiwa chepuo kurudi Mbeya City