Klabu ya Chelsea imeripotiwa kufikia makubaliano binafsi na kipa Andre Onana wakati huu wakitaka huduma yake ili akawa chaguo lao la kwanza langoni huko Stamford Bridge.

Lakini, ofa yao ya awali ya Pauni 34 milioni iliyopelekwa Inter Milan Imeripotiwa kugomewa.

Makipa Kepa Arrizabalaga na Edouard Mendy wamekuwa wakichuana kuwania Namba 1 huko Stamford Bridge kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita, lakini sasa Onana anataka kuja kuongeza nguvu.

Kipa Mcamerooni, Onana, 27 usiku wa Jumamosi (Juni 10) alikuwa golini wakati Inter Milan ilipokipiga na Manchester City kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na miamba hiyo ya Italia kukubali kichapo cha bao 1-0.

Tangu anatua Inter Milan mwaka jana, Onana alikuwa akihusishwa na mpango wa kuachana na timu hiyo na kinachoelezwa na Tutto Mercato, ameshakubaliana mambo binafsi na Chelsea.

Hata hivyo, The Blues imeshuhudia ofa yao ya awali ya Pauni 34 milioni kukataliwa na Inter.

Onana alisaini mkataba wa miaka mitano wakati anatua Inter na atakuwa kwenye kikosi hicho cha Italia hadi 2027.

Kwa urefu wa mkataba wake hiyo ina maana, Inter wanataka kuvuna pesa nyingi kwenye mauzo ya kipa huyo, huku ikielezwa dau la Pauni 40 milioni linaweza kutosha kumng’oa San Siro.

Tanzania inatambua, inaheshimu usawa wa kijinsia - Dkt. Mwinyi
Ukimwi: Mratibu wa kimataifa ateta na Rais Dkt. Samia