Klabu ya Tottenham Hotspurs imeripotiwa kumfukuzia Kiungo Mshambuliaji klabu ya Manchester United, Jadon Sancho katika dirisha hili la usajili ili kuboresha kikosi chao.

Sancho ambaye alijiunga na Man United mwaka 2021 anahitajika na klabu hiyo kutoka kaskazini mwa jiji la London ili kuhakikisha wanarudi kwenye ubora wao baada baada ya kuwa na msimu mbovu wa 2022/23.

Man United inaripotiwa kuhitaji kiasi cha euro milioni 60 ili kumuachia winga huyo wa ki- mataifa wa England.

Kama Tottenham watakubali kutoa kiasi hicho cha fedha ni wazi mchezaji huyo ataelekea Spurs msimu ujao.

Sancho tangu ajiunge ndani Man United amekua na kiwango cha kusuasua kitu ambacho kimefanya klabu hiyo kufikiria kumuuza kwani ni msimu wa pili sasa hajafanikiwa kuonesha ubora ambao alikuwa nao ndani ya Borussia Dortmund.

Man United ina mpango wa kuondoa wachezaji kadhaa klabuni hapo kuelekea dirisha hili kubwa ili waweze kusajili wachezaji wengine wenye ubora mkubwa.

Huku Jadon Sancho akiwa kwenye orodha hiyo hivyo klabu ambayo itafika bei wanayoitaka United mchezaji huyo atauzwa Spurs nao wakiwa ndio wako mstari wa mbele.

Azam FC: Tunakuja na kikosi kazi kazi
Mgawanyo jimbo la Mbeya: Dtk. Tulia amtaja Magufuli