Wataalam wa Wizara za kisekta, chini ya Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu wameanza uchunguzi wa Kiikolojia kuhusu Ugonjwa wa Virusi vya Marburg baada ya ugonjwa huo kutokomezwa Nchini unaofanyika Mkoani Kagera.

Mkurugenzi Msaidizi Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Ofisi ya Waziri Mkuu, Prudence Constantine amesema Ofisi ya Waziri Mkuu imeratibu sekta na Taasisi mbalimbali kufanya uchunguzi wa kiikolojia ili kubaini uwepo wa Wanyama wanaoweza kuhifadhi Virusi vya Marburg.

Amesema, utafiti huo pia utahusisha kujua mwingiliano wao na wanadamu ambapo Uchunguzi huu ni moja kati ya juhudi za pamoja za kuendelea kujua chanzo cha tatizo, kujiandaa, kukabiliana na dharura za kiafya ikiwemo endapo zitajitokeza.

“Wizara ya Afya imeainisha uchunguzi huu kati ya kazi muhimu zinazotakiwa kufanyika ndani ya mpango wa siku 90 wa kurejesha hali Mara baada ya mlipuko wa Marburg ulipotangazwa kuisha, ” amebainisha Prudence.

Namungo FC kujitathmini 2022/23
Erik Ten Hag: Victor Lindelof haendi kokote