Meneja wa Mabingwa wa Soka Barani Ulaya Manchester City, Pep Guardiola amewaonya Real Madrid kuwa makini kwani ameanza kuwafukuzia katika kutwaa mataji ya UEFA.

Hii ni baada ya Jumamosi (Juni 10) Manchester City kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza.

Guardiola aliiongoza Man City kutwaa taji la kwanza la UEFA katika historia ya klabu hiyo, lakini yeye kama kocha akitwaa kwa mara ya tatu baada ya huko nyuma kutwaa akiwa na FC Barcelona.

Katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid ndiyo baba lao wakiwa wametwaa mataji hayo mara 14 ikizifunika klabu zote.

Guardiola amesema Madrid wanatakiwa kuwa makini kwani bado mataji 13 tu aweze kuwafikia.

Bosi huyo alinukuliwa akisema: “Real Madrid wanatakiwa kuwa makini, tupo nyuma kwa mataji 13, wanatakiwa kujua kwamba wakizubaa sisi tunakuja taratibu, tutawafikia.”

Davies: FC Barcelona walinikataa kisa Canada
Sudan: Watumia muda wa utulivu kuwazika jamaa zao