Rais wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Injinia Hersi Said, amepiga mkwara mzito kuhusu masuala ya usajili akiweka wazi kuwa jina lolote atakalopewa atafanyia kazi kuhakikisha anamleta mchezaji huyo.

Injinia Hersi alifanikisha madili ya wachezaji wengi ndani ya kikosi cha Young Africans akiwemo Stephane Aziz KI ambaye alikuwa anakipiga ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Aziz Ki alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Simba pamoja na Azam FC, jambo lililoongeza presha kwenye kuisaka saini yake na mwisho aliibuka Young Africans.

Injinia Hersi amesema: “Kwenye suala la usajili, Young Africans tupo tofauti na tunazidi kuiboresha sekta hii kutokana na kuwa na mfumo wa mabadiliko, hivyo wakishafanya mchakato wao ninawaambia tu jina lolote wanipe.

“Wakinipa jina la mchezaji ambaye wanamuhitaji popote kule hizo ndizo kazi zangu, nitahakikisha ninakamilisha hilo dili na kuwapatia mchezaji wao.”

Bandari Tanga haitafutiwi muwekezaji - Waziri Mbarawa
Azam FC: Tunakuja na kikosi kazi kazi