Uongozi wa Simba SC umeweka wazi kuwa umeingia sokoni kuleta mtambo wa mabao utakaoongeza kasi kwenye idara hiyo kwa msimu wa 2023/24.
Ipo wazi kuwa Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira aliomba kuongezewa kiungo mshambuliaji mwenye kasi kama Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.
Oliveira amesema kuwa anahitaji kuwa na kiungo kama Ntibazonkiza ili kuongeza nguvu kwenye eneo la kiungo mshambuliaji pale Ntibanzokiza anapokuwa hayupo fiti.
Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa hawatafanya makosa kwenye usajili kwa kuwa wanajua aina ya wachezaji wanaotakiwa.
“Wale wachezaji ambao wanatakiwa na benchi la ufundi hao watakuja na nimeona namna ambavyo tunafanya kazi kwa umakini tutaleta wachezaji wenye ubora ambao watakuwa na nafasi yakuleta ushindani kwenye kikosi.
“Kikubwa mashabiki wasiwe na mashaka wakati unakuja na tutafanya kazi kwa umakini kwani msimu huu tunajua hatujafanya vizuri hivyo tunajipanga kwa wakati ujao,” amesema Ahmed Ally