Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi katika Kijiji cha Magungu, Kata ya Mpendo, Wilaya ya Chemba na kukemea vikali uongozi
wa Kijiji kukusanya fedha kwa wananchi bila kufuata utaratibu.

Senyamule ameyasema hayo Juni 13, 2023 mara baada ya kufanya ziara yakukagua utekelezaji wa miradi ya boost katika Wilaya ya Chemba.

Amesema, “sijaona dhamira ya dhati katika ukamilishaji wa mradi huu kwa muda tuliokubaliana wa tarehe 30/6/2023, tumekubaliana sote kuwa miradi hii ikamilike kwa wakati lakini leo nimesikitishwa sana hatua hii ya ujenzi ambao uko katika hatua za awali” Senyamule amefafanua.

Aidha ameongeza kuwa, “katika mradi huu Chemba hamjafika hata asilimia 20 na mna siku 18 zimesalia, fedha zilitolewa kwa wakati mmoja nchi nzima, Wilaya nyingine za Mkoa wa Dodoma wako katika hatua za upauji, siko tayati kumuangusha Mhe. Rais, ujenzi ufanyike mchana na usiku” Senyamule ameagiza.

Majambazi wanne wauawa na Polisi, mmoja atoroka
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 14, 2023