Maafisa wa Polisi kwa kushirikiana na wale wa Idara ya upelelezi – DCI, nchini Kenya wamewauwa kwa kuwapiga risasi washukiwa wanne wa ujambazi, katika eneo la Mkwajuni barabara kuu ya Mombasa Malindi.

Maafisa hao wamefanikisha mauaji hayo baada ya kuwafuatilia majambazi hao waliokuwa kwenye gari dogo wakitoka upande wa Mombasa, majira ya saa tisa alfajiri ya Juni 13, 2023, huku jambazi mmoja akitoroka.

Katika tukio hilo, Polisi walipata bunduki moja aina ya AK-47 inayodaiwa kuibwa kwenye tukio la uvamizi wa benki ya Equity, tawi la Matuu, Kaunti ya Machakos Julai 2021.

Hata hivyo, Polisi nchini humo inasema msako mkali unaendelea ili kuweza kumkamata jambazi aliyetoroka na kwamba zoezi hilo litaendela ili kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unakuwepo.

Uchunguzi tukio la ajuza aliyefufuka kwenye Jeneza waanza
Wanaokusanya ushuru bila utaratibu kukiona - Senyamule