Jeshi la Polisi nchini Nigeria, limesema zaidi ya watu 100 wamekufa maji katika eneo la kaskazini baada ya boti iliyokuwa imebeba familia zilizokuwa zikirudi kutoka harusini, kuzama katika mto, polisi na maafisa wa eneo hilo wamesema Jumanne.

Ajali hiyo iliyotokea katika jimbo la Kwara, inadaiwa kuwa ya hivi karibuni ambapo inadaiwa kuwa ni jambo la kawaida kutokana na boti hizo kupakia watu kupita kiasi, kukiuka taratibu za usalama na mafuriko makubwa katika msimu wa mvua.

Ofisi ya Gavana jimbo la Kwara, ilisema bila kutoa maelezo ya ziada kuwa hadi sasa kuna vifo vya watu 103 na zaidi ya 100 wameokolewa huku msemaji wa Polisi wa jimbo la Kwara, Okasanmi Ajayi akisema wataendelea kutoa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo.

Hata hivyo, utafutaji wa miili na uokozi bado unaendelea na hii inamaanisha kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka na kwamba waathiriwa walikuwa wakirudi kutoka kwenye sherehe ya harusi wakielekea wilaya ya Patigi katika jimbo la Kwara.

Rais Dkt. Samia uso kwa uso na Wananchi Nyamagana
Bunge lalegeza vyuma marekebisho sheria huduma ya Habari