Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Brazil Neymar amesema kuhamia kwa Lionel Messi katika Klabu ya Inter Miami kutaubadilisha mchezo wa wa Ligi Kuu ya soka ya Marekani.

Juma lililopita, Messi alitangaza uamuzi wake wa kujiunga na Inter Miami mara tu mkataba wake na Paris Saint-Germain utakapomalizika mwishoni mwa mwezi huu.

Neymar, ambaye alicheza na Messi kule Barca na PSG, amechanganya hisia kuhusu uamuzi wa Messi, ambao anaouona kuwa usajili mkubwa zaidi katika historia ya miaka 27 ya soka la Marekani.

“Nina uhakika kwamba Messi atabadilisha ligi nchini Marekani,” alisema Neymar.

“Ninaamini ligi itakuwa maarufu zaidi. Kwa hiyo kila mmoja anapaswa kutumia fursa na kufurahia kumtazama akicheza kwa sababu kwa bahati mbaya hakuna kinachodumu milele.”

Messi alikuwa na ofa za kurejea klabu ya zamani ya FC Barcelona na angeweza kuhamia klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia, lakini hatimaye aliamua kujiunga na Inter Miami timu ambayo mmoja wa wamiliki wake ni David Beckham.

“Nina huzuni na furaha kwa wakati mmoja,” alisema fowadi huyo wa BrazĂ­l.

“Nilijua tayari. Messi ni mmoja wa marafiki zangu wa karibu, zawadi ambayo soka imenipa. Nilipata fursa ya kumfahamu, kucheza naye na kisha kujenga urafiki mzuri.

“Kwa hiyo, nilijua kwamba angeweza kuja hapa (Miami), na tulizungumza kuhusu hilo. Nilimwambia angefurahi sana jijini, kwa sababu ya mtindo wa maisha, fursa ya kuja kuishi na kucheza hapa Miami.”

Neymar amekuwa akiishabikia Miami Heat wakati wa Fainali za mpira wa kikaku wa Marekani, NBA.

Siku ya Ijumaa, alikuwa kwenye umati wa watu katika Kituo cha Kaseya na aliandamana na mchezaji mwenzake wa Brazil na mshambuliaji wa Real Madrid, Vinicius Junior wakati Heat ilipopambana na Denver Nuggets katika mchezo wa nne.

Dani Cadena apewa mkono wa kwaheri Azam FC
DKT. Tulia akutana kwa majadiliano na Rais wa IPU