Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Brazil Vinicius Júnior atavaa jezi maarufu namba saba ya klabu hiyo ambayo ilikuwa ikivaliwa na Gwiji Cristiano Ronaldo.

Vinicius, mwenye umri wa miaka 22 kwa sasa ametambulishwa kwa jezi namba 7 kwenye tovuti ya klabu hiyo, akirithi namba hiyo kutoka kwa Eden Hazard aliyeondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu wa 2022/23.

Nyota mwenzake wa kimataifa wa Brazil kwenye timu hiyo, Rodrygo sasa atavaa jezi namba 11 baada ya kuondoka kwa Marco Ansensio.

Vinicius alikuwa anavaa jezi namba 20 msimu uliopita na Rodrygo anavaa jezi namba 21.

Nyota hao wawili ni sehemu muhimu kwenye kikosi cha kwanza cha Madrid na kwa pamoja wamefunga mabao 19 Ligi Kuu ya Hispania na mabao 12 Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hazard alikuwa akivaa jezi namba 7 tangu anajiunga na klabu hiyo Julai mwaka 2019 mpaka anaondoka mwezi huu.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubeligiji aliamua kuvunja mkataba wake uliobakiwa mwaka mmoja baada ya kuwa na misimu minne mibovu ndani katika klabu hiyo.

Ronaldo alivaa jezi namba 7 kwa misimu minane kati ya mwaka 2009 na mwaka 2018, na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Real Madrid kwa kufunga mabao 450 na kushinda mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Huko nyuma jezi namba 7 ilishawahi kuvaliwa na mshambuliaji Raul Gonzalez, ambaye kwa sasa anakifundisha kikosi cha akiba cha timu hiyo, Emilio Butragueño ambae kwa sasa ni Mkurugenzi wa Mahusiano wa Real Madrid, Amancio Amaro ambae alikuwa rais wa heshima ya Real Madrid mpaka umauti wake Februari mwaka huu na Juan “Juanito” Gomez.

Onana aikamua Simba SC Milioni 189.5
Singida Big Stars yapigwa bei kwa masharti