Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar – TAMWA ZNZ, imesema inaungana na nchi nyingine barani Afrika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kwa kusisitiza ulinzi wa mtoto katika nyanja zote.

Kongamano hilo litafanyika Juni 15, 2023 kwa kuwashirikisha watoto, asasi za kiraia, taasisi za kiserikali, wazazi, walimu na viongozi wa dini ambapo kaulimbiu ya TAMWA ZNZ katika maadhimisho hayo ni “Matumizi Sahihi ya Kidijitali kwa Ustawi Bora wa Mtoto.”

Takwimu zilizotolewa mwezi Januari na ofisi ya mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zinaonesha kuwa jumla ya watoto 1, 173 waliathirika na vitendo vya udhalilishaji na ukatili mwaka 2022 kati ya matukio 1,360 yaliyoripotiwa.

Hatua hiyo imepelekea, TAMWA Zanzibar inasisitiza kwa taasisi zinazosimamia haki za watoto na jamii kwa kuangalia jinsi gani mtoto atalindwa dhidi ya vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia ambao huathiri mustakabali wa maisha yao kwa ujumla.

Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 16 ya mwezi Juni inatokana na mauaji ya kinyama waliofanyiwa watoto waliokuwa wakiishi katika kitongoji cha SOWETO nchini Afrika ya kusini na serikali ya Makaburu ya nchi hiyo Juni 16, 1976.

Katika siku hiyo, watoto hao waliandamana zaidi ya nusu maili wakidai haki ya kupewa Elimu bora na mazingira ya kufundishwa kwa lugha yao, ambapo kwa harakati hizo watoto zaidi ya 100 waliuawa na askari polisi wa utawala wa makaburu wa Afrika ya Kusini wakati huo.

Wafanyabiashara Austria waitwa kuwekeza nchini
Mudathir, Sure Boy waipiga kijembe Azam FC