Eva Godwin – Dodoma.

Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko – CPB,  imepanga kuhakikisha kuwa  mwaka 2023 – 2024  wanaboresha huduma katika viwanda kwa kuwa na mazao yenye ubora zaidi na kuhakikisha viwanda vinafanya kazi masaa 24 kwa kushirikiana na wakulima nchini.

Akizungumza katika kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari  mbalimbali Nchini kilichofanyika mkoani iringa June 11 – 12 Kaimu Mkurugenzi wa taasisi hiyo, John Maige amesema  cpb inajukumu la kununua nafaka na mazao mchanganyiko kwa wakulima kwa bei shindani  ili kuongeza thamani ya mazao.

Amesema, watajitahidi kuzalisha kwa kuhakikisha malighafi zinaandaliwa kwa wakati na kuongeza ufanisi katika kuhifadhi mazao na kubainisha kuwa, “tutaongeza uzalishaji wa viwanda vyetu kwa kuhakikisha malighafi zinaandaliwa kwa wakati na pia tutaongeza ufanisi katika kuhifadhi mazao mchanganyiko.”

Aidha, Kaimu Mkurugenzi huyo amesema wataongeza ufanisi kwenye utekelezaji wa Mkakati wa masoko katika kuhakikish bidhaa zinapatikana kwa wakati nchini na kuboresha upatikanaji wa bidhaa kwa kuendelea kuongeza viwanda mbalimbali katika kanda, ili bidhaa zipatikane kwa wingi na kwa wakati.”

Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko ilianzishwa Mwaka 2019 kwa sheria ya bunge namba 19 kwa lengo la kufanya majukumu ya biashara ya nafaka na mazao mchanganyiko ikiwa imeanza na tani ya mazao 2550 na hadi kufikia mwaka 2021 waliweza kununua tani  51,000 za mazao mbalimbali kama Mahindi, Mpunga, Mchele maharage na Ngano.

Mbwana Makata kusalia Ruvu Shooting
Rashford: Sijali mashabiki wanasema nini