Timu ya Taifa ya Brazil itacheza dhidi ya Hispania katika mechi ya kirafiki mwezi Machi 2023 kama sehemu ya kampeni ya kupinga ubaguzi wa rangi kumuunga mkono Vinicius Jr.

Mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Bernabeu jijini Madrid nyumbani kwa winga huyo wa Brazil Vinicius katika klabu ya Real Madrid.

Vinicius alilengwa kwa unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi mara kadhaa nchini Hispania alipokuwa akiichezea Real katika kampeni zilizopita.

“Hakuna nafasi ya matusi ya kibaguzi katika soka letu,” alisema rais wa Chama cha Soka cha Hispania, Luis Rubiales.

Rubiales na mwenzake wa FA (CBF) wa Brazil Ednaldo Rodrigues walizindua kampeni yao ya kupinga ubaguzi wa rangi chini ya kauli mbiu ‘Ngozi moja’.

Ni muhimu kuelewa kwamba adhabu kali zaidi inapaswa kutumika katika kesi za ubaguzi wa rangi na mamlaka ya soka, Faini haitoshi. Klabu zinahitaji kuwajibika pia.” amesema Rodrigues.

CBF lilikuwa shirikisho la kwanza la soka kupitisha vikwazo vikali zaidi kwa kesi za ubaguzi wa rangi, kama vile kukatwa kwa pointi katika msimamo wa ligi, kufungwa kwa viwanja au kufungiwa kwa mashabiki na wanachama wa klabu maisha yao yote.

“Tunahitaji kuongoza kampeni duniani kote kupigana na virusi hivi ambavyo vinaaibisha kila mtu katika soka.”

Brazil itacheza na Guinea huko Barcelona keshokutwa Jumamosi na Senegal huko Lisbon siku tatu baadae.

Tukio la hivi punde zaidi la Vinicius kudhalilishwa kwa ubaguzi wa rangi nchini Hispania lilikuja wakati Real Madrid ilipocheza na Valencia Mei.

Vinicius, ambaye kadi yake nyekundu kwa kufanya vurugu mwishoni mwa mechi ilifutwa, baadaye alisema ligi ya Hispania “ni ya wabaguzi.”

Azam FC kufanya usajili wa kishondo 2023/24
Chanzo ugomvi wa Nyerere, Karume chaanikwa