Serikali imesema, maamuzi ya kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi nchini ni jambo la hiyari na mtu yoyote hatalazimishwa kujiunga na vyama hivyo.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Nderianaga Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu CCM, Rehema Mwandabila.

Katika swali lake, Mwandabila alitaka kujua kauli ya Serikali juu ya kujiunga na uanachama wa vyama vya wafanyakazi kuwa ni hiyari, ili kusiwepo na ulazima wa kujiunga na vyama hasa kwa walimu.

Akijibi swali hilo, Naibu Waziri Ummy alisema, “Vyama hivi ni vya kihiyari lakini katiba zao ndio zinawabana pengine ujiunge au ukijiunga utafaidika na kunufaika na kipi, kwa hiyo siyo lazima mtu ajiunge na vyama hivi.”

Nasreddine Nabi atuwa Afrika Kusini
Jeshi la Taifa Stars laanikwa hadharani