Ole Gunnar Solskjaer amewekwa kwenye mpango wa klabu moja ya Championship na huenda akakabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo ikiwa imepita miezi 19 tangu alipofutwa kazi Manchester United, imeelezwa.

Solskjaer alifutwa kazi Man United mwaka 2021 baada ya msimu wa hovyo ambao ulishuhudia timu hiyo ikimaliza nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi na tangu wakati huo amekuwa hana kazi.

Ripoti zinafichua kwamba kocha huyo raia wa Norway ameshapata nafasi ya kurudi mzigoni.

Kinachoelezwa ni kwamba klabu hiyo inayopiga hesabu za kumchukua Solskjaer ni Leicester City, ambayo inataka kurejea kwenye Ligi Kuu England kwa haraka zaidi baada ya kushuka msimu uliomalizika hivi karibuni.

Solskjaer alitua Man United kuchukua mikoba ya Jose Mourinho kama kocha wa muda vizuri na kupoteza mkataba wa kudumu na kuisaidia timu hiyo kushika nafasi ya pili kwenye ligi msimu wa 2020-2021, ikiwa ni msimu bora kabisa kwenye ligi tangu alipostaafu Sir Alex Ferguson mwaka 2013.

Mabosi wa Leicester City wamevutiwa na mafanikio hayo na sasa wanataka kumpa kibarua hicho cha kuwarudisha kwenye Ligi Kuu England kwa haraka. Hata hivyo, si yeye peke yake aliyepo kwenye rada za Leicester City baada ya miamba hiyo kumfikiria pia, aliyekuwa kocha wa Chelsea, Graham Potter.

Lakini, shida ya Potter ni kwamba hayupo tayari kufanya kazi Championship, anahitaji kwenye Ligi Kuu England. Hivyo, Leicester wanamfikiria pia Scott Parker, ambaye huko aliwahi kuzipandisha Fulham na Bournemouth.

Mac Allister afichua kilichompeleka Liverpool
Kante kulipwa mshahara mnono Al-Ittihad